Nyota wa muziki nchini Mr. Seed anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Albamu yake “Black Child” ambayo tayari ina takriban wiki tatu tangu itoke rasmi.
Album ya “Black Child” ambayo ndio albamu ya kwanza ya Mr. Seed tangu aanze muziki imefanikiwa kufikisha zaidi ya Streams laki tano kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.
Ikumbukwe album ya Black Child kutoka kwa mtu mzima iliachiwa rasmi Septemba 13 mwaka huu wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto huku ikiwa na kolabo 9 pekee.