You are currently viewing BLACK MARKET RECORDS YAMTAKA PRODYUZA DADDY ANDRE KUFUFUA MUZIKI WA ANGELLA KATATUMBA

BLACK MARKET RECORDS YAMTAKA PRODYUZA DADDY ANDRE KUFUFUA MUZIKI WA ANGELLA KATATUMBA

Angella Katatumba ni moja kati wasanii ambao wamedumu kwenye tasnia muziki nchini uganda kwa muda mrefu.

Licha ya kuanza muziki miaka 15 iliyopita, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 amekuwa akipambana kuupeleka muziki wake kimataifa.

Wakati alikutana na prodyuza Daddy Andre mwaka wa 2018 walirekodi wimbo wa pamoja uitwao “Tonelabira” ambao ulikuja ukawa mkubwa sana nchini Uganda mwaka wa 2019.

Hata hivyo walikuja wakakosana vibaya baada ya wawili hao kuchanganya raha ya mapenzi na muziki, jambo lilompelekea Angella katatumba kusuasua kimuziki.

Sasa taarifa mpya mjini ni kwamba lebo ya muziki ya Black Market Records imetoa rai kwa prodyuza Daddy Andre kumshika tena mkono Angella Katatumba  kama njia kufufua muziki wake.

Kulingana na chanzo cha karibu na lebo ya Black Market, Daddy Andrea ana mpango wa kumtayarishia Angella Katatumba nyimbo nne kali mwaka  huu wa 2022 ambazo zitakuwa moto wa kuotea mbali.

Utakumbuka wawili hao kwa sasa wana wimbo wa pamoja uitwao “Wendi” ambao unafanya vizuri kwenye chati mbali mbali nchini uganda.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke