You are currently viewing Bobi Mapesa kuachia album yake mpya Desemba mwaka huu

Bobi Mapesa kuachia album yake mpya Desemba mwaka huu

Msanii wa mkongwe kwenye muziki nchini Bobi Mapesa ametangaza ujio wa album yake baada ya ukimya wa miaka mitatu.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mapesa amesema kwa sasa yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya album yake mpya ambayo ana mpango wa kuichia Disemba 25 mwaka huu.

Bobi Mapema ambaye allikuwa anaunda kundi la The Bugz pamoja na msanii mwenzake VBO amesema Album hiyo iitwayo “Mapesa ndio Kabisa 2” itakuwa na jumla ya nyimbo 17 ya moto huku akiwashirikisha wasanii mbali mbali Afrika Mashariki.

Hitmaker huyo wa “Naskia Utamu” amesema album hiyo itakuwa ya pili kwake kama msanii wa kujitegemea ikizingitiwa ana album iitwayo Mepesa ndio Kabisa na nyingine mbili ambazo ameshirikishwa na wasanii Calvo Mistari pamoja na VBO iiitwayo Mawezere na BC mtawalia.

Lakini pia amezungumzia chanzo cha ukimya wake kwenye muziki kwa kusema kuwa amekuwa akijikita zaidi kwenye shughuli ya kuwafuga mbwa, biashara ambayo imekuwa ikimuingizia kipato zaidi tofauti na muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke