Mwanamuziki aliyegeukia siasa Bobi Wine ameibuka na kudai kuwa anatamani historia ya mwanamuziki Mozey Radio ijumuishwe kwenye mtaala wa shule za upili na msingi nchini Uganda.
Kulingana na Bobi Wine, kizazi cha sasa na kijacho kitapata fursa ya kujifunza mengi kuhusu maisha ya mwendazake Radio ambaye ni mwanamuziki wa muda wote kuwahi kutokea nchini uganda kutokana na kipaji cha kipekee alichokuwa nacho kipindi cha uhai wake.
Bobi Wine amesema utawala wa sasa nchini Uganda unaogopa kuwapa nafasi wanafunzi mashuleni kujifunza kuhusu maisha ya mwanamuziki Mozey Radio kwa sababu wana hofu ya kuikuza kizazi kitakachopinga udhalimu unaoendelezwa serikali.
Hata hivyo amesema akishika hatamu ya uongozini miaka zijazo atawatangaza hadharani wanamuziki Mozey Radio na Herman Basude kama mashujaa wa tasnia ya muziki nchini uganda.