You are currently viewing BOOMPLAY KUANDAA WARSHA YA WASANII JIJINI NAIROBI DESEMBA MOSI 2021

BOOMPLAY KUANDAA WARSHA YA WASANII JIJINI NAIROBI DESEMBA MOSI 2021

App namba moja kwa huduma ya muziki barani Afrika, Boomplay inatarajiwa kuandaa makala ya pili ya kila mwaka ya muziki ambayo yanalenga kuwaunganisha wasanii na kukuza tasnia ya muziki nchini.

Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba mosi mwaka huu itawaleta pamoja zaidi ya washikadau 80 wa muziki wakimemo maprodyuza, wasanii, mameneja, lebo za muziki na watunga sera ili kujadili changamoto zinazozikabili tasnia ya muziki nchini pamoja na suluhu ya kudumu ya kuboresha muziki wa Kenya.

Katika taarifa yake mkurugenzi mkuu wa Boomplay Afrika Mashariki, Martha Huro,amesema wamehamua kuja na jukwaa hilo ili kubadilishana mawazo na wasanii kuhusu namna ya kuongezea wafuasi na pia njia za kuwaingiza kipato kupitia kazi zao za muziki.

Makala ya mwaka huu ya jukwaa la wasanii Boomplay yamethaminiwa na kinywaji cha Hennessy na wawakilishi kutoka mashirika kama MCSK, PRISK, na wadau wengine wa muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke