You are currently viewing BOOMPLAY WATOA ORODHA YA WASANII WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2021

BOOMPLAY WATOA ORODHA YA WASANII WALIOFANYA VIZURI MWAKA 2021

Mtandao wa kusikiiza na kuratibu kazi za wasanii wa muziki Boomplay Kenya umetoa orodha ya jumla ya wasanii walio fanya vizuri ndani ya mwaka huu 2021.

Kulingana na boomplay Kenya top 3 ya wanamuziki wa kike walioongoza kwa kusikilizwa zaidi katika mtandao huo nchini,inaongozwa na Nadia Mukami akiwa na streams millioni 14.7 akifuata kwa ukaribu na Mercy Masika ambaye ana streams millioni 6.9 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Slyvia Ssaru ambaye ana streams millioni 3.5.

Kwa upande wa wasanii wa kiume waliosikilizwa nchini Otiile Brown anaongoza akiwa na streams millioni 42.5, Bahati anashikilia nafasi ya pili na streams millioni 25.2 huku Willy Paul akifunga tatu bora na streams millioni.

Sanjari na hilo Otile Brown, Nadia Mukami na Bahati wametajwa kama Wasanii waliotafutwa zaidi nchini kwa mwaka huu wa 2021 katika mtandao wa Boomplay huku Mr Seed, Ndovu Kuu na Nikita Kering wakitajwa kuwa wasanii waliokuja kwa kasi kwa mwaka huu wa 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke