Rapa kutoka Marekani Bow Wow amekuwa akijiita Baba wa mtoto mmoja kwa kipindi cha miaka 10 ambayo amekuwa na binti yake Shai Moss.
Hivi karibuni alikuwa akikataa maswali ya kuwa na mtoto mwingine, kupitia ukurasa wake wa twitter, aliwahi kukanusha kwa kusema ana mtoto mmoja tu.
Kwa mujibu wa mitandao mbali mbali, Bow Wow alikuwa akimkataa mtoto wa Olivia Sky hadi kushindwa kumpa msaada wa pesa za matunzo hadi pale ambapo Mahakama ilipofikia uamuzi wa kuthibitisha kuwa rapa huyo ni Baba halali wa mtoto huyo wa Kiume, Stone Moss mwenye umri wa mwaka mmoja.
Bow Wow mwenye umri wa miaka 34, ameridhia na kuamua Kutangaza rasmi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa sasa ni Baba wa watoto wawili.