You are currently viewing BOW WOW AMKANA HADHARANI PRODYUZA JERMAINE DUPRI

BOW WOW AMKANA HADHARANI PRODYUZA JERMAINE DUPRI

Rapa kutoka Marekani Bow Wow anaendelea kumkana prodyuza Jermaine Dupri ambaye wote tunaamini ana mchango mkubwa kwenye maisha ya muziki ya rapa huyo. Bow Wow ameibuka na kusema Dupri hapaswi kupewa sifa zozote kwamba alihusika katika kumtoa kimuziki, bali sifa zote ziende kwa Snoop Dogg ambaye alimvumbua na kumpa jina.

Hayo yameibuka baada ya shabiki mmoja kupitia twitter kusema “Snoop anaweza kuwa aligundua kipaji chake lakini Jermaine Dupri alimtengeneza na kuwa Bow Wow” kauli ambayo ilimfanya kuibuka Bow Wow na kukanusha vikali.

Bow Wow alienda mbali zaidi na kusema hakuna album wala wimbo wowote ambao anauzimia kipindi anafanya kazi na Jermaine Dupri.

“Alimtengeneza nani? Hahaha aliwatengeneza Kris Kross, Hakunitengeneza mimi. Sikupitia kufundishwa namna ya kuwa msanii na wala sikufundishwa namna ya kuchana (Ku-rap) Nilikuja kwenye game nikiwa tayari. Simkosei heshima lakini hakunifundisha chochote kuhusu hii biashara ya muziki. Na huo ndio ukweli, huwa hatoi ushauri.” aliandika Bow Wow akimjibu shabiki huyo.

Utakumbuka Kipaji cha Bow Wow kiligunduliwa na Snoop Dogg mwishoni mwa miaka ya 90 na kisha kuchukuliwa na Jermaine Dupri ambaye alimsaini chini ya label yake, ya So So Def Recordings

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke