Timu ya Taifa ya Brazil imesonga mbele katika hatua ya Robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuitandika Korea Kusini 4-1 katika uwanja wa 974 mjini Doha.
Bao la kwanza la Brazil lilifungwa na Venicius Jr dakika ya 7 ya mchezo huo, Neymah Jr alipachika bao la pili katika dakika ya 13 naye Richarlison aliongeza bao la tatu katika dakika ya 29 na Lucas Paqueta alimalizia bao la 4 katika dakika ya 36.
Kwa upande wao Korea Kusini walipata bao la kufutia machozi katika dakika ya 76 Paik Seung-Ho.
Wakati huo huo Timu ya Taifa ya Croatia imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia baada ya kuiondosha Japan kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3 kwa 1 baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya 1-1
Mlinda lango wa Croatia Dominic Livakovic ndiye aliyeibuka shujaa kwenye mchezo huo kwa kudaka penati 3
Kwa sasa Brazil watakutana na Croatia katika hatua ya robo fainali