You are currently viewing BREEDER LW ADOKEZA UJIO WA KOLABO YAKE NA KUNDI LA UNCOJINGJONG

BREEDER LW ADOKEZA UJIO WA KOLABO YAKE NA KUNDI LA UNCOJINGJONG

Baada ya kufanya vizuri na singo yake “Gin ama Whiskey” akiwa ameshirikiana na staa wa muziki nchini Mejja, Rapa Breeder LW amedokeza ujio wa kolabo nyingine akiwa na kundi la muziki linalokuja kwa kasi kwa sasa Uncojingjong.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Breeder LW amepost picha ya pamoja akiwa na wasanii wa kundi hilo ambapo amewataarifu mashabiki zake wakae mkao wa kula kupokea remix ya wimbo uitwao “Wanjapi” kutoka kwa Unco jing jong.

“Piga Luku Kula Wanjapi@uncojingjong @litttlemaina_#BigBaba #bazengamentality #wanjapi”,Ameandika Breeder LW

Kukazia hilo kundi la Unco jing jong limethibitisha kufanyika kwa Remix ya wimbo huo kupitia mitandao ya kijamii huku wakiambatanisha na video wakiwa studio na Breeder LW wakiimba sehemu ya wimbo wa ‘Wanjapi”

“WANJAPI 2 LOADING Different artists different tastes…Tushaa skia wa East (@rapdokta & @is_bullet )…Acha tuskie wa West

#wanjapi #ajingjongneverdie”..Uncojinjong wameandika kupitia Instagram.

Kwa mujibu wa taarifa yao, Remix ya ‘Wanjapi’ itaingia rasmi sokoni wiki hii.

Mpaka sasa wimbo wa ‘Wanjapi” kutoka kwa Unco jing jong unazidi kufanya vizuri kwenye majukwaa mbali mbali ya kupakua na kusikiliza mtandaoni kwani ndani ya miezi tisa imefanikiwa kufikisha zaidi ya views laki 2 youtube.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke