Habari nzuri kwa mashabiki wa muziki nchini ni kwamba tutarajie muda wowote ujio wa Collabo kati ya Exray na Rapper Breeder LW.
Breeder LW amethibitisha taarifa hiyo kwa mashabiki kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni ambapo amewataka mashabiki kukaa mkao wa kula kupokea wimbo huo.
Iwapo Breeder Lw na Exray wataachia collabo yao hiyo itakuwa ni kazi yao ya kwanza kufanya pamoja ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma wamekuwa wakikutana kwenye kazi za wasanii wengine.
Ikumbukwe Breeder Lw anafanya vizuri na singo yake mpya “Gin ama Whisky ambayo amemshirikisha Mejja na mpaka sasa video yake ina views million 1.2 kwenye mtandao wa youtube ndani kipindi cha wiki tatu.