You are currently viewing BRIANA AMTOA HARMONIZE KWENYE ULIMWENGU WA ANDROID

BRIANA AMTOA HARMONIZE KWENYE ULIMWENGU WA ANDROID

Mpenzi wa Harmonize, Briana amemzawadi bosi huyo wa lebo ya muziki ya Konde Gang Worldwide simu aina ya i-Phone 13.

Harmonize amethibitisha hilo kupitia InstaStory yake kwenye mtandao wa Instagram ambapo ameonyesha kuanza kutumia simu aina iphone kwa mara ya kwanza. 

Hitmaker huyo wa “Teacher” amempongeza mpenzi wake mpya Briana kwa kusema kwamba amekuwa chachu ya yeye kuanza kutumia simu hiyo aina ya iphone 13 kutoka kwenye ulimwengu wa Android ambao amekuwa akitumia siku zote.

Ikumbukwe Briana kutoka Australia anakuwa mwanamke wa pili mwenye asili ya kizungu kuwa kwenye mahusiano na Harmonize, kwani awali alikuwa kwenye ndoa na Sarah Michelloti kutoka Italia kabla ya ndoa yao kuvunjika.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke