You are currently viewing BRITNEYS SPEARS APEWA UHURU WA KUMILIKI MALI ZAKE

BRITNEYS SPEARS APEWA UHURU WA KUMILIKI MALI ZAKE

Baada ya miaka 13 kupita bila kuwa na uhuru na mali zake hatimaye mwanamuziki kutoka nchini Marekani Britney Spears amepewa uhuru na mahakama

Mwanamuziki huyo nguli duniani aliwekewa kizuizi cha maamuzi juu ya mali zake na baba yake mzazi Jamie Spears kupitia mahakama ya nchini humo, mnamo mwaka wa 2008 kotokana na kushindwa kujimudu kimwili na kiakili kutokana na msongo wa mawazo alioupata baada ya kuachana na mume wake Kevin Federline.

Hakimu aliyetambulika kwa jina la Brenda Penny November 12 amempa uhuru wa akaunti zake za benki, na mali zake zote kwa kuwa kwa sasa anaonekana kurudi kwenye hali ya kawaida ya kumudu maisha yake. Pamoja na maamuzi hayo jaji Brenda amemteua John Zabel kusimama kama msimamizi wa baadhi ya mambo ya Britney akichukua nafasi ya baba mzazi wa staa huyo

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke