You are currently viewing BROWN MAUZO AACHIA RASMI V ALBUM

BROWN MAUZO AACHIA RASMI V ALBUM

Mwanamuziki kutoka Kenya Brown Mauzo ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la V.

V album imebeba jumla ya mikwaju 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 5 pekee.

Brown Mauzo amewashirikisha wasanii mbali mbali kama Masauti, Baraka the Prince,Ndovu Kuu, Mwasi, na Kaa La Moto.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mauzo amesema ameachia album yake ya v kama zawadi kwa mke wake Vera Sidika ambaye juzi kati amejifungua mtoto wa kike aitwaye Princess Asia Brown.

Album ya “V” ni album ya pili kwa mtu mzima Brown Mauzo baada ya Nitulize ya mwaka wa 2019.

Hata hivyo Album hiyo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya  kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke