You are currently viewing BROWN MAUZO ATAMANI VERA SIDIKA AMZALIE WATOTO WENGI ZAIDI

BROWN MAUZO ATAMANI VERA SIDIKA AMZALIE WATOTO WENGI ZAIDI

Staa wa muziki nchini Brown Mauzo amedai kwamba anataka kupata watoto wengi na mke wake Vera Sidika ambaye ni Socialite maarufu Afrika Mashariki.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Mauzo amewataka wakenya wamsaidie kumshawishi mrembo huyo ili aweze kufanikisha azimio lake la kupata watoto wengi nae.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wameonekana kufarahishwa na kauli hiyo ya mtu mzima Brown Mauzo wengi wakimtaka apambane na hali yake kwani ni vigumu kwao kuingilia mambo ya watu wawili ambao tayari wamezama kwenye penzi nzito.

Ikumbukwe juzi kati Brown Mauzo na mke wake Vera Sidika walibarikiwa na mtoto wa kike aitwaye Asia Brown ambapo Brown mauzo alienda mbali zaidi na kuachia album iitwayo V kama zawadi kwa Vera Sidika kumzalia mtoto mrembo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke