You are currently viewing BRUNO K NA BINTIYE BRIELLA WALAMBA SHAVU LA UBALOZI IMPERIAL LEATHER UGANDA

BRUNO K NA BINTIYE BRIELLA WALAMBA SHAVU LA UBALOZI IMPERIAL LEATHER UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Bruno K pamoja na binti yake Briella wamelamba dili nono la ubalozi wa kampuni ya Imperial Leather.

Bruno K amethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare baadhi ya picha zikiwaonyesha wakitia sahihi mkataba wa maelewano na uongozi wa kampuni ya Imperial Leather.

Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali nchini Uganda wameonekana kumpongeza Bruno K pamoja na mwanae Briella kwa mafanikio hayo makubwa maishani huku baadhi wakimponda msanii huyo kwa kumtumia vibaya binti yake kujipatia pesa wakati huu angali mdogo.

Ikumbukwe mwezi mmoja uliopita Bruno K alimpoteza baby mama wake Rachel Nasasira baada ya kuagua kwa muda mrefu. Baada ya kifo chake kulikuwa na ripoti kuwa msanii huyo alikatazwa kumchukua binti yake Briella kutokana na hatua ya kumtelekeza baby mama wake akiwa hai.

Lakini baadae alifanikiwa kumtorosha binti yake kutoka kwa mama ya mke wake kitu ambacho kiliibua mzozo mkali kati yake na familia ya baby mama wake wa wakimtuhumu kwa hatua ya kumrubuni mtoto huyo bila ya ridhaa yao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke