You are currently viewing BUCHAMAN ATOA ONYO KWA WATOTO WA KIKE DHIDI YA UAVYAJI MIMBA

BUCHAMAN ATOA ONYO KWA WATOTO WA KIKE DHIDI YA UAVYAJI MIMBA

Msanii mkongwe kutoka nchini Uganda Buchaman amewaonya wasichana wadogo dhidi ya uavyaji mimba akisema maamuzi hayo ni hatari sana kwa maisha yao.

Msanii huyo amewashauri wanawake kujifungua kila mara wanapopata mimba na kuchukua tahadhari za usalama zinazohitajika wakati wa uja uzito.

Hitmaker huyo wa “Thank you” ametoa mfano wa jinsi mkewe Claire Naganjja almaarufu kama Mama Ghetto alivyojifungua salama bila changamoto yoyote alipochukua ushauri wa daktari kuhusu ujauzito.

Buchaman amewaonya wanawake dhidi ya kitendo hicho cha kikatili alipokuwa akielezea furaha yake baada ya mke wake kujifungua mtoto wa kiume wiki chache zilizopita.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke