Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Buchaman alifurushwa nyumbani kwake mapema wiki iliyopita kutokana na malimbikizi ya kodi ya zaidi ya miezi sita.
Kutokana na hilo Mwanamuziki huyo kwa sasa ametoa wito kwa serikali ya uganda kumnusuru kwani hana matumaini kama atapata pesa za kulipa kodi bila usaidizi wa serikali.
Buchaman ameenda mbali zaidi na kusema kuwa biashara zake zote ziliathiriwa na msala wa corona, hivyo hana chanzo kingine cha kumuingizia kipato ikizingatiwa kwamba hapati tena riziki kutoka kwa muziki wake kwani tasnia ya muziki nchini uganda bado imefungwa.
Buchaman kwa sasa na familia yake wamekita kambi kwa rafiki yake eneo la Luwaffu, viungani mwa jiji la Kampala.
Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mzima Buchaman kwenye nyumba za kupanga,kwani kipindi cha nyuma alifukuzwa kwa nguvu kwenye nyumba aliyokuwa akiishi huko Namungo, nchini Uganda baada ya kushindwa kulipa kodi.