You are currently viewing BURA BOY ATIANI, AHUSIKA NA MAUJI YA WATU NIGERIA

BURA BOY ATIANI, AHUSIKA NA MAUJI YA WATU NIGERIA

Staa wa muziki wa Nigeria Burna Boy ameingia kwenye msala mzito mno wa mauaji.

Kwa mujibu wa Polisi wa Lagos nchini Nigeria, wanawashikilia maafisa watano wa Polisi wenye ukaribu na Burna Boy kwa tuhuma ya kuwapiga risasi watu wawili kwenye Klabu ya Cubana usiku wa Juni 8, mwaka huu.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa, Polisi hao wanaomlinda Burna Boy walifika kwenye klabu hiyo na staa huyo ambaye alikwenda moja kwa moja kwenye sehemu ya VIP akiwa na wanawake watatu.

Lakini wakiwa wanaendelea na starehe, Burna Boy alimuona mwanamke mwingine mzuri ambapo bila kujua ni mke wa mtu, alimtuma Polisi mmoja amshawishi mwanamke huyo ili aungane naye kwenye kula bata.

Hapo ndipo kulipotokea vurugu kubwa ambapo mmoja wa maafisa hao wa Polisi alimpiga risasi ya paja mume wa mwanamke huyo na mtu mwingine kichwani na wanaendelea na matibabu baada ya kutolewa risasi mwilini. Inaelezwa kwamba wakati risasi zikipigwa, Burna Boy alikuwa akiamrisha wapigwe risasi huku akifurahia.

Hata hivyo, mara baada ya tukio hilo, Burna Boy anadaiwa kutorokea nchini Hispania ambapo anasakwa ili akamatwe kwa msala huo huku Polisi hao wawili wakiwa nyuma ya nondo za mahabusu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke