Mwanamuziki kutoka Nigeria Burna Boy ameachia rasmi orodha ya ngoma zinazopatikana kwenye album yake mpya ya Love Damini ambapo ina jumla ya ngoma 19 ikiwa na collabo 9 pekee.
Mkali huyo ambaye Julai 2 alisherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, amewapa mashavu wasanii kama J Balvin, Ed Sheeran na wengine wengi kwenye album yake hii mpya. Album hiyo inatoka Julai 8, Ijumaa ya wiki hii.
“Love Damini” inakuwa ni album ya sita kwa Burna Boy baada ya kupata mafanikio makubwa na album yake ‘Twice as Tall’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2020.