You are currently viewing BURNA BOY AKAVA JARIDA LA ES MAGAZINE LA NCHINI UINGEREZA

BURNA BOY AKAVA JARIDA LA ES MAGAZINE LA NCHINI UINGEREZA

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria  Burna Boy ambaye anafanya vizuri kupitia kazi zake mbalimbali, ametokea mbele ya kava la Jarida la Es Magazine la nchini Uingereza.

Jarida la Evening Standard Magazine ni jarida kutoka London, Uingereza ambalo hujihusisha kwa kutoa habari za burudani kutoka kwa mastaa wakubwa ulimwenguni.

Kwenye Jarida hilo Burna Boy  amefunguka mengi kuhusiana na muziki wake, mpaka kufikia hapo alipo. Uwezo wake mkubwa wa kujaza kwenye Arena, dili mbalimbali alizozipata kama PEPSI, kukutana na mastaa wakubwa, kushiriki kwenye album za wasanii kutokea Marekani.

Hata hivyo, Burna boy  anakuwa msanii wa tatu kutoka Afrika kupata nafasi ya kukava jarida la ES, mwaka 2019 WizKid alikava Jarida hilo na mwaka 2020 ikawa zamu ya Davido kutokea kwenye jarida hilo.

Ikumbukwe, Burna Boy kupata nafasi ya kukava kwenye jarida hili kubwa ulimwenguni kunampa nafasi ya kuzingatiwa, kuongeza mashabiki na watu kupata nafasi ya kuweza kumfuatilia zaidi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke