You are currently viewing BURNA BOY AKIRI LAST LAST NDIO WIMBO ULIOMUINGIZIA PESA NYINGI KATIKA MUZIKI WAKE

BURNA BOY AKIRI LAST LAST NDIO WIMBO ULIOMUINGIZIA PESA NYINGI KATIKA MUZIKI WAKE

Burna Boy ameweka wazi kwamba wimbo wake “Last Last” umemuingizia pesa nyingi zaidi kuliko wimbo wake wowote ambao amewahi kuutoa. Wimbo huo ambao unapatikana kwenye album yake mpya ‘Love Damini’ uliachiwa rasmi mwezi Mei mwaka huu.

Aidha asilimia 60 ya mapato ya wimbo huo yanaenda kwa Mwanamuziki wa Marekani Toni Braxton kwa kutumia kionjo cha wimbo wake ‘Not Man Enough’ wa mwaka 2000.

Hata hivyo wimbo wa “Last Last” umeingia rasmi kwenye Chart za Billboard Hot 100, ngoma hiyo imechumpa na kukamata nafasi ya 86 kwenye chart hiyo wiki hii.

Huu unakuwa wimbo wa kwanza kwa Burna Boy kufikia mafanikio makubwa kwenye chart hizo na pia ndio ingizo lake la kwanza. Aidha Album yake mpya (Love Damini) imechumpa hadi nafasi ya 14 kwenye chart za bora, Billboard 200.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke