You are currently viewing Burna Boy ashinda tuzo ya Msanii Bora MTV Europe Music Awards 2022

Burna Boy ashinda tuzo ya Msanii Bora MTV Europe Music Awards 2022

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Burna Boy ameshinda tuzo ya MTV Europe Music Awards (MTV EMA) 2022 kama Best African Act.

Hiyo ni baada ya kuwabwaga Tems na Ayra Star, wote kutokea Nigeria, pia kuna Musa Keys wa Kenya, Black Sherif wa Ghana na Zuchu wa Tanzania.

Tuzo hizo zimetolewa usiku wa kuamkia leo Novemba 14, 2022 katika ukumbi wa PSD Bank Dome huko Duesseldorf, Ujerumani ikiwa ni mara ya sita kwa nchi hiyo kuwa mwenyeji.

Utakumbuka hii ni Tuzo ya pili kwa Burna Boy, alishinda tena Tuzo hiyo mwaka 2019.

Tuzo hizo zinazotolewa na Paramount International Networks kuheshimu wasanii na muziki katika utamaduni wa Pop, tangu mwaka 2007.

Hadi tuzo za mwaka 2021, Justin Bieber ndiye anashikilia rekodi ya kushinda tuzo nyingi zaidi zikiwa ni 22, huku msanii wa kike anayeongoza akiwa ni Lady Gaga aliyeshinda 12. Kwa upande wa makundi, BTS ndio vinara upande wa wanaume wakishinda 14, huku upande wa wanawake, Little Mix waking’ara na tuzo saba.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke