Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria Burna Boy amesema kwamba ni vyema sheria ikaruhusu matumizi ya bangi nchini humo kwani haina madhara kama ambavyo wengi wanasema.
Akihojiwa kwenye kipindi cha ‘Home Grown Radio’ jijini Los Angeles, Burna ameeleza kwamba watu wengi wanatumia bangi lakini hawataki kutangaza hadharini lakini kiukweli hamna madhara mabaya yoyote mtu akitumia.
“Kila mtu anatumia bangi lakini hakuna anayetaka kusema au kukutwa nayo.” amesema Burna Boy.
Lakini pia Hitmaker huyo wa Kilo metre amesema watu wazima na viongozi wamefanikiwa kutoa elimu kwa jamii kwamba endapo mtu akitumia bangi basi atakuwa chizi jambo ambalo yeye amelikataa na kusema kuwa ni uongo, hivyo ni bora sheria iruhusu matumizi ya bangi.