You are currently viewing BURNA BOY AWAKOSOA MASHABIKI KUHUSU MAPOKEZI YA WIMBO WAKE “LAST LAST”

BURNA BOY AWAKOSOA MASHABIKI KUHUSU MAPOKEZI YA WIMBO WAKE “LAST LAST”

Mwanamuziki wa Nigeria Burna Boy amejitokeza kukosoa mashabiki zake kwa jinsi wamepokea wimbo wake uitwao “Last Last”.

Kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa Tik Tok Burna Boy amesema watu wanafurahia wakichezea wimbo huo ilhali ni wa maumivu ya mapenzi.

Ujumbe huo umewaaminisha walimwengu kuwa huenda mwanamuziki huyo anapitia wakati mgumu kuhusiana na maswala ya mapenzi jambo lilomsababisha kuandika na kuimba wimbo huo.

Mwezi Januari mwaka huu burna boy alisema kwamba hataki tena kuwa na hisia kama binadamu na alikuwa tayari kulipa kiasi chochote cha fedha kwa yeyote ambaye angesaidia kumwondolea hisia.

Lawama zake ziliambatanishwa na tukio la mwanamuziki huyo kuachana na mpenzi wake Stefflon Don ambaye pia ni mwanamuziki wa nchini Uingereza.

Uvumi kuhusu kutengana kwa wawili hao ulisheheni mitandaoni mwezi Disemba mwaka 2021 na siku chache baadaye Burna Boy akathibitisha kupitia Instagram ambapo aliandika kwamba yeye hana mke.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke