Msanii kutoka Nigeria Burna Boy ameendelea kurushiana maneno na mashabiki wa Wizkid, kupitia mtandao wa Twitter ameshambuliana nao tena hadi kutishia kumpiga Wizkid.
Burna Boy alijikuta akiingia kwenye vita hiyo ya maneno baada ya mashabiki wa Wizkid kumvamia kwenye tweet yake ambayo aliweka mafanikio ya Album zake.
Baada ya mashabulizi ya maneno kutoka kwa Wizkid FC, Burna Boy alikuja na kumwambia shabiki mmoja “Kama Wizkid asingekuwa rafiki yangu, basi kiukweli ningempiga ngumi ya uso papo hapo ili mashabiki zake wa Twitter wafahamu kwamba Mimi sio Davido. Lakini namshkuru Mungu ninafahamu na nimepevuka sana kufahamu (Wizkid) sio wewe.” aliandika Burna Boy kwenye tweet ambayo tayari imefutwa.