You are currently viewing BURNA BOY AWATOLEA UVUVI MASHABIKI WA WIZKID KWA KUMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

BURNA BOY AWATOLEA UVUVI MASHABIKI WA WIZKID KWA KUMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

Kumeibuka vita kati ya Burna Boy na mashabiki wa WizKid (Wizkid FC) kwenye mtandao wa Twitter. Burna Boy amewatupia vijembe kwamba wamekuwa wakimzushia vitu vya kijinga na kumtengenezea stori ambazo hazina ukweli wowote, na hii yote ni kutokana na kukosa elimu.

“Niliwahi kusema kitu kama hichi kipindi cha nyuma lakini wafuasi wadanganyifu wa Wizkid (Wizkid FC) walisema nadanganya. Labda kama history ilikuwa inafundishwa kwenye shule zenu. Wizkid anapaswa kuwa na watu nadhifu hapa Twitter badala ya wajinga kama hawa.” aliandika Burna Boy na kuweka picha ya shabiki mmoja wa Wizkid.

Shabiki mmoja alimuuliza kama zile insta stories zilizosambaa toka kwa Offset na ile iliyoonekana imetoka kwa Stefflon Don, zina ukweli? Burna Boy alijibu hapana, bali zilitengenezwa na mashabiki wapuuzi wa Wizkid FC.

Burna alikuwa akiunga mkono kitu kilichosemwa na Professor aitwaye Wole Soyinka juu ya kuondolewa somo la Historia ya Nigeria kwenye mitaala ya elimu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke