Burna Boy ametangaza rasmi onesho lake ambalo litafanyika katika ukumbi mkubwa na maarufu wa Madison Square Garden uliopo New York nchini Marekani.
Onesho hilo ‘One Night In Space’ litafanyika April 28 mwaka 2022 ambapo Burna Boy ataweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza toka Afrika kuibariki steji hiyo kama msanii kinara.
Uongozi wa Madison Square Garden pia umeutumia ukurasa wao wa Instagram kutangaza onesho hilo na tiketi zitaanza kuuzwa mnamo Disemba 16.
Ukumbi wa MSG una uwezo wa kubeba watu 20,789. Justin Bieber ndiye anashikilia rekodi ya kuujaza ukumbi huo kwa haraka zaidi, show zake mbili za ‘Believe Tour’ zilikuwa Sold out ndani ya sekunde 30 mwaka 2012.
Kabla, mwanadada Taylor Swift ndiye alikuwa akishikilia rekodi hiyo kwa kuujaza kwa sekunde 60 mwaka 2009