Kundi la muziki nchini Kenya, Buruklyn Boyz limeachia rasmi Album yao mpya inayokwenda kwa jina la East Mpaka London..
Album hiyo ambayo ina jumla ya mikwaju 16 ya moto ina kolabo 3 kutoka kwa wakali kama Young Louie, Maya Amolo na Silverstone Barz.
East Mpaka London Album ina nyimbo kama Pree, Blicky, Coins,Ex, Delete, Taliban na inapatikana exclusive kupitia digital platforms mbalimbali za kupakua na kusikilizia muziki duniani ikiwemo,Youtube, Apple Music na Spotify.
Album hii ni ya kwanza kwa wasanii wa Buruklyn Boyz tangu waanze safari yao ya muziki miaka mitatu iliyopita.
Buruklyn Boyz ni kundi la muziki wa Drilll ambalo linaundwa na wasanii Mr. Right pamoja na Ajay na lilipata umaarufu nchini mwaka wa 2019 lilipoachia singo yao ya kwanza iitwayo “Durag na Slice.”