Rapa kutoka Marekani Cardi B ameongeza rekodi nyingine kwenye historia ya muziki wake.
Mrembo huyo amekuwa rapa wa kwanza wa Kike kufikisha nyimbo mbili ambazo zimefikia hadhi ya Diamond yaani zimeuza nakala milioni 10 kwa nchini Marekani.
Cardi B amefikia mafanikio hayo kupitia ngoma alioshirikishwa na Maroon 5 iitwayo ‘Girls Like You’ iliyotoka mwezi Mei mwaka wa 2018. Wimbo wake wa kwanza kugonga Diamond ulikuwa ‘Bodak Yellow’ mwezi March mwaka huu.