You are currently viewing Cardi B afunguka uoga kuathiri muziki

Cardi B afunguka uoga kuathiri muziki

Rapa Cardi B ameingiwa na hofu, na hiyo ndio sababu kuu ambayo inamfanya achelewe kuachia Album mpya kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

Cardi B anasema amekuwa muoga kuachia ngoma kutokana na watu kumkosoa sana.

“Kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 nilikuwa napenda Muziki, lakini kwa sasa, kufanya muziki kwangu mimi imekuwa Kazi ambayo inanifanya niwe na wasiwasi.

Kwa sababu kila mmoja anakosoa kila kitu ninachofanya. Wakati mwingine hupaswi kufanya kitu ambacho kinakufanya uwe na wasiwasi.” alisema Cardi B.

Tangu alipoachia Album yake ‘Invasion of Privacy’ mwaka 2018, Cardi B amekuwa akirekodi nyimbo lakini haridhishwi na anachokifanya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke