You are currently viewing CARDI B AMKINGIA KIFUA MUMEWE OFFSET KWA UGOMVI WA BURNA BOY NA WIZKID

CARDI B AMKINGIA KIFUA MUMEWE OFFSET KWA UGOMVI WA BURNA BOY NA WIZKID

Rapa Cardi B ameibuka na kumkingia kifua mume wake Offset baada ya kusambaa kwa post ambayo inaonesha Offset akisema kwamba tayari ana ngoma na Burna Boy.

Hii ni kufuatia kushindwa kumpata Wizkid kutokana na kutoza pesa nyingi kwenye kolabo ikilinganishwa na Burna Boy.

Sasa baada ya wengi kuliiwekea post hiyo mashaka Cardi B ameibuka na kupuzilia mbali madai hayo kwa kusema kwamba hayana ukweli wowote kwani haitajatoka kwa Offset.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Cardi B ameandika “Fake As F*ck” na kisha kuifuta Tweet hiyo.

Utakumbuka baada ya post  inayodaiwa kuwa ya Offset akimzungumzia Wizkid na Burna Boy kusambaa mtandaoni, taswira mbaya ilijengeka miongoni mwa walimwengu wengi wakihoji kuwa Burna Boy ni msanii wa kawaida kifedha ukimlinganisha na Wizkid.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke