You are currently viewing CARDI B AMZAWADI OFFSET CHEQUE YA SHILLINGI MILLIONI 226

CARDI B AMZAWADI OFFSET CHEQUE YA SHILLINGI MILLIONI 226

Wakati ukichukulia poa kumbukizi ya kuzaliwa kwa mpenzi wako, huko nchini Marekani rapa Cardi B hakuwa na jambo dogo kwa Baby Daddy wake OffSet , Hitmaker huyo wa “WAP” amemsurprise mume wake Offset kwa cheque nzito ya dollar million 2 za Kimarekani kama zawadi ya Birthday yake ambayo ilikuwa Disemba 14.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa instagram Offset ametoa shukrani za dhati kwa mke wake Cardi B kwa zawadi hiyo ya kitofauti ambayo hakuitegemea, sambamba na kuonyesha mkoba huo pamoja na bei kupitia risiti ya manunuzi.

“Wow Asante mpenzi (Cardi B). Mara nyingi unaniletea vitu vya kitofauti nakupenda na nakuheshimu sana”. Aliandika Offset kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hii sio mara ya kwanza kwa Cardi B kumpa mumewe zawadi kubwa  kwani mwaka 2020 wakati Offset aliposherehekea kutimiza miaka 29, Cardi B alimsurprise na ndinga kali,aina ya  Lamborghini Aventador SVJ.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke