Rapa Cardi B kutoka Marekani ameendelea kuwa mtu wa ahadi kwa mashabiki wa muziki wake juu ya ujio wa album yake mpya baada ya miaka mitatu sasa.
Jana kupitia Instagram LIVE, Cardi B amesema watu watarajie album mpya wakati wowote kuanzia mwaka 2022.
Sababu kuu ya kuchelewa kuachiwa kwa album hiyo ni muda, Cardi B amedai kwamba amekuwa na muda finyu ukizingatia kwa sasa ana watoto wawili.
Invasion of Privacy ya mwaka 2018 ndio album pekee ambayo Cardi B amewabariki mashabiki zake tangu atie mguu kwenye muziki.