Female Rapper kutoka Marekani Cardi B ametoa maoni yake kuhusu nchi ya Urusi na ameshauri viongozi wakubwa duniani watafute suluhisho kwa usalama wa raia.
Hii inakuja baada uwepo wa machafuko ya kisiasa yanayoendelea kati ya Ukraine na Urusi.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Cardi B anasema inabidi waanze kufikiria namna ambavyo raia wanaathirika kutokana na maamuzi yao.
Lakini pia amesema kutokana na dunia kukumbwa na majanga kadhaa, viongozi hao wasiyape kipaumbele masuala ya kuwekeana vikwazo, vita, na kuvamiana.