Mpenzi wa zamani wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Sonie amekanusha taarifa za kurudiana na mchekeshaji huyo.
Hii ni baada ya Mulamwah kuposti video jana kupitia ukurasa wa Instagram na kuandika ujumbe ulioashiria kuwa wamerudiana jambo lilowaaminisha walimwengu wawili hao wamezika tofauti zao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sonie amesema madai ya mulamwah hayana msingi wowote huku akisisitiza kuwa hawajasuluhisha mgogoro uliopo kati yao kama inavyoripotiwa mitandaoni.
Mrembo huyo amesema Mulamwah alitokea ghafla na kuivamia shughuli zake za kupiga picha na ndipo akataka wazungumzie nae jambo analodai lilipelekea kitu k mapaparazi kuchukua video akiwa na mchekeshaji huyo.
Hata hivyo amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kupumzilia mbali taarifa za kurudiana ambapo mbali zaidi na kumtaka mulamwah aombe familia, mashabiki pamoja binti yao msamaha kwa kumzushia madai ya uongo.
Utakumbuka katika kipindi cha wiki moja iliyopita Mulamwah alikamata headlines za habari mtandaoni baada ya kujitokeza na kudai kwamba aliachana baby wake Carol Sonie mwaka wa 2021 baada ya mrembo huyo kumsaliti kimapenzi kwa kuzaa na mwanaume mwingine ambapo alienda mbali zaidi na kudai kuwa Keilah Oyando sio mtoto wake.