You are currently viewing CAROL SONNIE AMJIBU KIMAFUMBO BABY DADDY WAKE MULAMWAH

CAROL SONNIE AMJIBU KIMAFUMBO BABY DADDY WAKE MULAMWAH

Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carrol Sonnie amefunguka kwa mara ya kwanza siku chache baada ya Mulamwah kuibua kashfa nzito dhidi yake.

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram ameandika ujumbe wa mafumbo ambao umetafsiriwa  na walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuwa inamlenga moja kwa moja mpenzi wake wa zamani mulamwah.

“Wakati maisha inakupa sababu mia moja ya kuangua kilio na kuhuzunika, una jukumu la kuonesha maisha sababu millioni moja ya kutabasamu na kushukuru. Baki na nguvu,” Ameandika Caroll Sonnie kupitia Instastory yake.

Utakumbuka juzi kati Mulamwah aliibuka kupitia mitandao yake ya kijamii na kufunguka mengi kuhusu maisha yake ya ndani kwa kusema kwamba alivunja mahusiano yake na Carol Sonnie baada ya mrembo huyo kumsaliti kimapenzi kwa kutoka na mwanaume mwingine.

Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kumkana mtoto aliyezaa na Carol Sonnie kwa kusema kuwa sio wake kwa kusema mtoto huyo sio wake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke