You are currently viewing CARTOON 47 ALALAMIKA KUTENGWA KWENYE MAFANIKIO YA WIMBO WAKE MPYA

CARTOON 47 ALALAMIKA KUTENGWA KWENYE MAFANIKIO YA WIMBO WAKE MPYA

Msanii Cartoon 47 ameonesha kutoridhishwa na mapokezi ya wimbo wake mpya uitwao Haiwezi ambao amemshirikisha Stevo Simple Boy na Ntosh Ngazi.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Cartoon 47 amesema watu wamekuwa wakimchukulia stevo kama mmiliki wa wimbo huo wakati yeye ndiye aligharamia mchakato wa kutayarisha wimbo wenyewe kwa kumleta Ntosh Gazi kutoka Afrika Kusini.

Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kwamba jambo hilo limepelekea baadhi ya mapromota kuanza kumpendelea Stevo  kwenye shoo zao huku wakimtenga.

Hata hivyo ametoa wito kwa wadau wa muziki nchini kutomchukulia poa kwenye muziki wake na badala yake watambua pia mchango wake kwenye mafanikio ya wimbo huo.

Wimbo huo uitwao Haiwezi wenye mahadhi ya Amapiano unafanya vizuri kwenye majukwaa mbali mbali ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni ambapo kwenye mtandao wa youtube ina zaidi ya views laki 1 ndani siku 5 tangu iachiwe rasmi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke