Mchekeshaji aliyegeukia muziki Cartoon Comedian ameachia rasmi wimbo wake mpya uitwao “Mbona Unacheat” wiki kadhaa baada ya kutangaza kuwa ameachana na mpenzi wake.
Wimbo huo ambao uliachiwa rasmi Oktoba 23, video yake imefanikiwa kufikisha zaidi watazamaji laki moja kwenye mtandao wa Youtube .
Kuachiwa kwa wimbo wa “Mbona Unacheat” umekuja siku moja baada ya Cartoon Comedian kumrushia vijembe Vera Sidika kuwa anapaswa kufuata nyayo zake za kuwekeza kwenye muziki mzuri badala ya kufanya kiki mtandaoni.
Utakumbuka Septemba 24 mrembo huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka wazi kuumizwa kimapenzi baada ya mchumba wake kukimbia ambapo alienda mbali zaidi na kusindikiza ujumbe wake ns hashtag mbona unacheat ambayo kisadfa imegeuka kuwa wimbo.
Cartoon alianza safari yake ya muziki mapema mwaka huu, ambapo ameachia jumla ya nyimbo mbili ambazo ni Kamkora na Acheni Jokes.