Mchekeshaji aliyegeukia muziki Cartoon Comedian ameweka wazi gharama aliyotumia kutayarisha video ya wimbo wake mpya ambayo itaingia sokoni leo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mrembo huyo amejinasibu kuwa alitumia kiasi cha shillingi millioni 2.5 kufanikisha mchakato mzima wa kuiandaa video ya wimbo wake mpya.
Haikushia hapo ameenda mbali zaidi na kumtolea uvivu mrembo vera sidika kwa kumtaka awekeze kwenye muziki wake baada ya kujihusisha matukio yasiokuwa na tija kwa mashabiki zake.
“MY MUSIC VIDEO HAD COST ME 2.5MILLION IT’S WORTH THE WAIT…DROPPING TODAY @7pm…AMBIENI VERA MUSIC NI INVESTMENT!!!! Wait for me”, Ameandika.
Hata hivyo kauli ya Cartooon Comedian imezua gumzo mtandaoni ambapo walimwengu wamezushia kila aina matusi na kumtaka aache majigambo ikizingatiwa kuwa hana kipaji kwenye faini ya muziki na ucheshi mtawalia.