You are currently viewing CATHARINE KUSASIRA ATAKA SERIKALI YA UGANDA KUMRUHUSU BOBI WINE KUTUMBUIZA

CATHARINE KUSASIRA ATAKA SERIKALI YA UGANDA KUMRUHUSU BOBI WINE KUTUMBUIZA

Mwanamuziki kutoka Uganda Catherine Kusasira ametoa wito kwa serikali ya nchini hiyo kumruhusu Bobi Wine kutumbuiza kwenye majukwaa ya muziki.

Katika mahojiano yake hivi karibuni kusasira amesema ni wakati muafaka kwa bobi wine kurudi kwenye muziki kwa kuwa siasa zilikamilika kwani ndiyo chanzo kuu iliyomfanya azuiwe kutumbuiza kwenye majukwaa ya burudani.

Aidha amesema kuwa Bobi Wine alizuiwa kutumbuiza kwa sababu alichanganyika muziki na siasa, jambo ambalo lilizua mvutano katika yake na serikali.

 “Siasa ziliisha na Bobi Wine hana budi kuanza tena kazi yake ya muziki. Naamini sababu iliyomfanya kufungiwa kuimba ni siasa kwani alitumia muziki kutangaza ajenda zake za siasa.

Kusasira ametoa kauli hiyo kufuatia mapokezi mabaya ambayo amekuwa akiyapata kwenye shoo zake ambazo alipangiwa kutumbuiza.

Utakumbuka ni takriban miaka minne sasa tangu Bobi Wine apigwe marufuku kutumbuiza kwenye maeneo ya umma baada ya kutangaza  nia ya kuchuana na Rais Museveni kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke