Mapromota wa muziki nchini Uganda wameacha kumzingatia msanii wa bendi Catherine Kusasira kwenye shoo zao, kwa hofu kuwa huenda akazua fujo na kupelekea matamasha yao ya muziki kutofanya vizuri.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Kusasira amesema hofu hiyo inatokana na mwelekeo wake wa kisiasa.
“Si rahisi kwa mapromota kunishirikisha kwenye shoo zao. Siasa zimeathiri biashara zetu,” amesema
“Niko katika kiwango ambacho lazima niombe promota anipee nafasi kwenye shoo au niwasihi mashabiki waje kwenye onesho langu,” ameongeza.
Utakumbukwa Catherine Kusasira ni mfuasi mkubwa wa chama tawala nchini Uganda NRM na mwaka wa 2021 alikuwa moja ya kati wasanii waliomkingia kifua Rais Yoweri Museveni kutua uongozi wa nchi hiyo.