Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Catherine Kusasira amekanusha madai ya kuwadharau watu mitandaoni baada ya kuonekana akijigamba na vibandu vya pesa.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Kusasira amedai kitendo chake cha kuwaonesha mashabiki kibunda cha pesa mtandaoni ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya tamasha lake la muziki kuzungumziwa mtandaoni na sio vinginevyo.
Mrembo huyo amesema pesa hizo alikopeshwa na promota Baalam kwa ajili ya kufadhili tamasha lake la muziki, hivyo hakuwa na nia ya kuwavunjia heshima mashabiki.
Kauli yake imekuja mara baada ya mashabiki kumshambulia mtandaoni alipokiri kuwa nyumba yake inapigwa mnada hivi karibuni kutokana na madeni anayodaiwa na benki.