You are currently viewing Celine Dion agundulika na ugonjwa usiotibika

Celine Dion agundulika na ugonjwa usiotibika

Mwanamuziki mkongwe Celine Dion mwenye umri wa miaka 54 ameweka wazi hali ya afya yake kwa kusema amegundulika ana ugonjwa usiotibika unaofahamika kama Stiff Person Syndrome (SPS), ambao ni ugonjwa wa neva.

Celine Dion ambaye amejizolea umaarufu mkubwa duniani kote amewaambia wafuasi wake milioni 5.2 wa mtandao wa Instagram kuwa, ugonjwa huo unaifanya misuli yake isimame bila kudhibitiwa na amekuwa akikabiliana na ugonjwa huo kwa muda mrefu.

Mara kadhaa ugonjwa huo umesababisha mwanamuziki huyo nguli raia wa Canada kushindwa kutembea na hata kuimba, hali itakayomlazimu pia kuahirisha kushiriki kwenye maonesho yaliyopangwa kufanyika Ulaya mwezi Februari mwaka 2023.

“Hivi majuzi nimegunduliwa kuwa na ugonjwa wa nadra sana wa Neva unaoitwa Stiff Person Syndrome ambao kwa wastani huathiri mtu mmoja kati ya milioni moja.
Kwa bahati mbaya, mikazo hii inaathiri kila nyanja ya maisha yangu ya kila siku, wakati mwingine husababisha ugumu ninapotembea na kutoniruhusu kutumia sauti zangu kuimba jinsi nilivyozoea.” amesema Celine

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke