Sakata la Willy Paul kudaiwa kununua matatu ambayo imetumika imechukua mkondo mpya baada ya bosi wa Bonfire Adventures Simon Kabu kukiri hadharini yeye ndio mmiliki halisi wa matatu hiyo.
Kupitia posti ya msanii Willy Paul kwenye mtandao wa Instagram Kabu ameandika ujumbe wa kumpongeza msanii huyo kwa hatua ya kuwekeza kwenye biashara ya matatu ambapo ameenda mbali zaidi na kujinadi kuwa kabla ya Willy Paul kununua matatu hiyo yeye ndio alikuwa anamiliki.
Ujumbe huo umezua hisia mseto mitandaoni ambapo baaadhi ya wakenya wameonekana kumkosoa Kabu kwa madai ya kumvunjia heshima Willy Paul huku wengine wakiendelea kumponda msanii huyo wakihoji kuwa walikuwa na fahamu kuwa matatu hiyo ishatumika.