Tume ya uchaguzi katika Chama cha Wanamuziki nchini Uganda (UMA) hatimaye, imetangaza tarehe mpya ambayo uychaguzi sambamba na mdahalo wa wagombea wa urais katika chama hicho utafanyika.
Hapo awali, mdahalo huo ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu lakini haukufanyika kwa sababu zilizokuwa nje ya tume hiyo.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi katika chama cha UMA Bwana. Jeff Geoffrey Ekongot ameeleza kuwa mjadala huo utafanyika Mei 21 kabla ya zoezi la upigaji wa kura kung’oa nanga Mei 23 mwaka huu.
Uongozi wa chama cha UMA hata hivyo umeshindwa kufafanua ikiwa upigaji kura katika chama hicho utafanyika kwa njia ya kidijitali, au kwa mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye vituo vya kupiga kura.
Utakumbuka wasanii King Saha na Cindy Sanyu wanatarajiwa kumenyana kwenye kinyang’anyiro cha urais katika chama cha uma ambapo mshindi katika uchaguzi huo ataongoza chama hicho kwa miaka miwili na nusu.