Nguli wa muziki kutoka nchini Uganda Jose Chameleone amekuwa akifanya kazi ya muziki kwa takriban miongo mitatu bila kupoa.
Baada ya kuachia nyimbo kali zilizokonga nyoyo za wapenzi wa muziki mzuri Afrika Mashariki, mkali huyo wa ngoma ya “Mama Mia” ametangaza kuchukua mapumziko ya miezi mitatu kwenye muziki wake.
Vyanzo vya karibu na Jose Chameleone,vimedai kuwa msanii huyo amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kusafiri nchini Marekani kuonana na familia yake kwani mara ya mwisho kutua nchini humo ilikuwa mwaka wa 2019.
Taarifa hii inakuja mara baada ya bosi huyo wa Leone Island kupata VISA ya kwenda nchini Marekani wiki kadhaa zilizopita.