You are currently viewing CHAMELEONE AFUNGUKA CHANZO CHA UGOMVI WAKE NA BOBI WINE

CHAMELEONE AFUNGUKA CHANZO CHA UGOMVI WAKE NA BOBI WINE

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Jose Chameleone amekiri hadharani kwamba hana uhusiano mzuri na msanii mwenzake Bobi Wine ambaye aligeukia siasa.

Akiwa kwenye moja ya onesho lake huko Kyengera Chameleone amedai kuwa Bobi wine alimnyima tiketi ya kugombea wadhfa wa umeya wa jiji la kampala kupitia chama chake cha NUP kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini uganda.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Forever” amesema jambo hilo lilimfanya apoteze imani kwenye siasa na sasa ameamua kuelekeza nguvu zake zote kwenye muziki kwani ni kitu anachokifahamu kwa undani.

“Sitaki kumzungumzia alininyima tiketi ya chama chake. Nimepoteza imani kwenye wadhfa wa umeya. Kwa sasa nimelekeza nguvu zangu kwenye muziki kitu ninachokifahamu kwa undani,” Alisema.

Chameleone ambaye ni bosi wa Lebo ya muziki ya Leone Island amesema anajihisi mwenye furaha zaidi akiwa karibu na wasanii kama Bebe Cool, Eddy Kenzo na David Lutalo na wengine wengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke