You are currently viewing CHAMELEONE AFUNGUKA KUHUSU BIFU YAKE NA BOBI WINE

CHAMELEONE AFUNGUKA KUHUSU BIFU YAKE NA BOBI WINE

Msanii mkongwe nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka uhusiano wake na Bobi Wine ambaye wamekuwa kwenye bifu kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Chameleone amesema kwa sasa hana ugomvi wowote na msanii huyo aliyegeukia siasa kwa kuwa alishamsamehe zamani kwa hatua ya kunyima tiketi ya chama chake cha nup wakati alikuwa anawania wadhfa wa umeya wa jiji la kampala.

“I have no problem with Bobi Wine and I cleansed my heart for whatever he did. I didn’t get the party ticket but I don’t mind about that anymore.” Amesema.

Hitmaker huyo wa Forever ameeleza kuwa hawezi kubali  siasa iharibu uhusiano wake na Bobi Wine ambao wameujenga kwa kipindi kirefu ikizingatiwa kuwa wamekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa zaidi ya miaka 20.

“I have known Bobi Wine for twenty years and our relationship matters most,” he said in an interview with local television.” Ameongeza

Utakumbuka Chameleone na Bobi Wine mara ya mwisho kukutana ilikuwa kwenye birthday party ya mwanamuziki mwenzao Eddy Yaawe ambayo ilifanyika mwezi meo mwaka huu viungani mwa jiji la Kampala.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke