You are currently viewing CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOWANIA URAIS UMA

CHAMELEONE AFUNGUKA SABABU ZA KUTOWANIA URAIS UMA

Msanii mkongwe nchini Uganda Jose Chameleone amevunja ukimya wake kuhusu kutowania urais katika chama cha wanamuziki nchini humo UMA.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Chameleone amesema ameshikika sana kwenye kazi zake za muziki hivyo atapata nafasi ya kutekeleza majukumu ya chama cha wanamuziki nchini Uganda.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Forever amedai kuwa wasanii wanahitaji mtu ambaye ameshikika kikazi lakini pia ana muda wa kujishughulisha na majukumu ya chama hicho.

“I would have contested to be UMA President but honestly am very busy for that. We need to find artists that are busy but can run the post as well”, –Jose Chameleone.

Hata hivyo hajabainika ni lini hasa uchaguzi wa chama cha wanamuziki nchini Uganda utafanyika baada ya Wizara ya Leba, jinsia na masuala kijamii kuahirisha uchaguzi huo bila kutoa maelezo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke